Kuelekea mchezo wa UEFA kesho Chelsea vs Barcelona





UEFA champions league kulindima viwanja viwili tofauti usiku wa kesho nchi mbili tofauti lakin macho ya wengi yana elekezwa nchini Uingereza tofaut na Ujerumani ambako mchezo moja utapigwa kati ya mabingwa wa nchi hiyo Baryen münchen na Besiktas ya Turkey.

Chelsea fc anawakaribisha Fc Barcelona katika mchezo wa UEFA champions league apo kesho tarehe 20 mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Stanford bridge uku Chelsea akiwa na rekodi nzuri zaidi kuliko Barcelona.

Katika michezo 12 walio kutana Chelsea ameonekana mbabe Kwa Barcelona baada ya kushinda michezo 4 kutoa sare 5 na Barcelona akishinda Mara 3 tu uku wote wakiwa na idadi Sawa ya magoli 18.

Hata hivo watu wamekosa imani na klabu ya Chelsea wakizani ina mwendelezo mbaya wa michezo yake lakin michezo mitano ya mwisho kabla ya mchezo huu ameshinda 4 na kupoteza 1 na nikwa mabao kuanzia 3 lakini upande wa Barcelona ameshinda michezo 3 na kusare 2 Kwa wastani wa mabao 2.

Nyota wa mchezo huo ambao watu wanatarajia kuona nini wata Fanya Kwa upande wa Chelsea Eden hazard na Alvaro morata upande wa Fc Barcelona ni Leonel mess na Luis Suarez.


<<<endelea kuwa na ezesports Kwa habari moto za michezo na burudani>>>

Comments

Popular posts from this blog

Star's kuvaana na wa Algeria na DR Congo

Watakao cheza nusu final UEFA champions league kufahamika wiki hili